Language

Ugonjwa wa Kifua kikuu (TB) huandamana kwa karibu sana na ugonjwa wa UKIMWI na malaria na ni mojawapo ya magonjwa yanayosababisha vifo Vingi nchini Tanzania, Tanzania ni kati ya nchi 30 zenye viwango vikubwa vya maambukizi ya Kifua kikuu na kifua kikuu / UKIMWI. Mkakati wa USAID dhidi ya kifua kikuu nchini Tanzania. unasaidia Mpango wa Taifa wa kupambana na Kifua Kikuu na Ukoma (NTLP) kushughulikia changamoto za kimfumo na kiutendaji kuzuia, kugundua, na kutibu ugonjwa huu. Hii ni pamoja na kuboresha upatikanaji wa huduma bora, inayozingatia wagonjwa wa Kifua kikuu, Kifua Kikuu / Ukimwi, na Kifua Kikuu sugu; kuzuia maambukizi na mwenendo wa ugonjwa; na kuimarisha majukwaa ya kifua Kikuu ya Tanzania kupunguza utegemezi wa ufadhili wa nje wa kifedha na kitaalamu.