Language

Serikali ya Tanzania imedhamiria, kwa watu wake na kwa jamii ya kimataifa, kuboresha utawala bora na wa kidemokrasia. Ingawa Tanzania bado iko juu ukilinganisha na nchi jirani kwa suala la uwazi, uwajibikaji, na haki za kiraia, kushuka kwa kasi kwa demokrasia katika miaka ya hivi karibuni kunaashiria wasiwasi. USAID inasaidia katika kuboresha hayo kwa kutekeleza miradi ambayo imejengwa siku za nyuma yenye kutoa majibu ya kukabiliana na kushuka kwa nafasi za kiraia na kisiasa, kukuza uhuru wa kujieleza, kuboresha utetezi na uwezo wa mawasiliano wa taasisi za kiraia , mashirika ya ndani, kukuza mifumo ya uwazi na uwajibikaji isiyo na rushwa, na kuimarisha haki za binadamu katika jamii, hasa kwa wale walio hatarini.