Language

Kwa kushirikiana na Taasisi ya Jane Goodall (JGI), mradi wa utunzaji wa ardhi magharibi mwa Tanzania, unafanya kazi ya kulinda Sokwe walio hatarini, pamoja na kulinda makazi yao kwa kutumia namna mbalimbali, kama mipango ya matumizi bora ya ardhi, kuwawezesha wananchi kuwa na maisha bora katika vijiji vinavyozunguka Gombe, Masito na Ugalla. Maeno ya Gombe –Massito –Ugalla yanakadiriwa kuwa na sokwe zaidi ya asilimia tisini ya idadi yote ya sokwe takribani 2,200 walioko ukanda wa magharibi mwa Tanzania.