Language

Jifunze Uelewe ni mradi wa miaka minne ambao unalenga kuendeleza uboreshaji wa kusoma, kuandika na kuhesabu kwa wanafunzi wote katika elimu ya awali na msingi. Tanzania imeshuhudia ukuaji wa kasi ya upatikanaji wa elimu ya msingi, lakini matokeo na ubora wa elimu na ufundishaji yanabaki kuwa chini kuliko nchi zingine. Tangu kuanzishwa kwa elimu ya bila malipo ya ada, idadi ya walimu imeshindwa kuendana na ongezeko la mahitaji ya wanafunzi, hasa kutoka kwa watoto wenye ulemavu.