Language

Vijana wa Kitanzania wana uwezo wa kuchangia jukumu muhimu katika maendeleo ya uchumi wa nchi yao, lakini zaidi ya vijana 800,000 wanaoingia katika nguvukazi ya Tanzania kila mwaka, ajira bado ni changamoto. Ili Tanzania ifaidike kwa kuongezeka kwa idadi ya vijana na kufikia malengo ya ajenda yake ya maendeleo, ni muhimu zaidi sasa kuliko hapo awali kuwapa vijana ujuzi, mafunzo, na rasilimali wanazohitaji kuchangia uchumi. Karibu 67% ya nguvukazi nchini Tanzania wanajishughulisha na kilimo. Nchi, inashughulikia ukosefu wa ajira kwa kuhamasisha vijana kuwa na utaalam zaidi katika sekta hiyo. Mradi wa Feed the Future Inua Vijana nchini Tanzania, unaunganisha vijana kupata mafunzo ya ujasiriamali, ujuzi wa kitaalam katika stadi za maisha, uongozi, pamoja na kilimo bora chenye kuzingatia afya, na fursa za ajira. Mradi huu unakusudia kuongeza fursa za mapato kwa vijana 21,500 kupitia mafunzo yakinifu, ya kitaalam na kuwaunganisha vijana kwenye ajira zilizo rasmi na zisizo rasmi.