Language

Serikali ya Marekani imetoa dola milioni 12 (TZS 28 bilioni) kusaidia vijana wa Kitanzania katika kuanzisha, kuendesha na kuwekeza katika biashara ya kilimo bara na Zanzibar. Tangazo hilo lilitolewa na Balozi wa Marekani nchini Dkt. Michael A. Battle na Mkurugenzi Mkazi wa USAID/Tanzania Bi. V. Kate Somvongsiri katika hafla za uzinduzi wa Mradi wa Feed the Future - Uimarishaji Sekta Binafsi Zanzibar na Dodoma.