Language

DAR ES SALAAM - Serikali ya Marekani, kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) ilkabidhi vifaa vya UVIKO-19 kwa Wizara ya Afya ya Zanzibar.

Mradi wa USAID wa Mnyororo wa Ugavi wa Afya Duniani hivi karibuni ulinunua vifaa vya upumuaji  na usafi wa mazingira vyenye thamani ya Dola za Marekani  $400,000. Vifaa viliwasilishwa mwezi uliopita Bandari ya Zanzibar na kusambazwa kwenye vituo vya umma vya kutolea huduma za afya kupitia bohari kuu ya madawa. Shehena hiyo inajumuisha vifaa vya kupumulia kama vile vipimo vya mwenendo wa damu, mirija ya kupimia puani kwa watoto na watu wazima, barakoa; na vifaa vya usafi wa mazingira kama vile dawa za mkoba za kunyunyizia, na mifuko ya kuwekea taka hatarishi.

Akizungumzia kuhusu utoaji wa vifaa tiba, Dk Abdullah S. Ali, Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto, Zanzibar alisema "Tunaamini katika uhusiano wa ushirikiano ambao unatoa huduma bora za afya kwa watu wote. Shehena ya vifaa tiba vilivyopokelewa vitaziba mapengo yaliyopo katika kupunguza hofu inayohusishwa na tishio la UVIKO- 19 kwa suala la vifo, maradhi na kulazwa hospitalini. ”

Serikali ya Marekani imejitolea kufanya kazi bega kwa bega na washirika wote katika sekta ya afya ya Tanzania ili kupunguza athari za UVIKO-19. Marekani ndiye mfadhili mkuu duniani kimataifa katika kukabiliana na  UVIKO-19, na zaidi ya mwaka jana, Kwa kipindi cha mwaka mmoja sasa, Marekani imetoa Dola za Marekani milioni 16.4 kupunguza UVIKO-19 nchini Tanzania.

Balozi wa Marekani nchini Tanzania Donald Wright alisema kuwa Serikali ya Marekani inafurahi kushirikiana na Wizara ya Afya ya Zanzibar kutoa vifaa hivi muhimu.


"Mchango wetu wa vifaa vya kupumua na vya usafi vyenye thamani ya Dola za Marekani 400,000 ni ishara ya kujitolea kwetu kwa ushirikiano huu, na tunatarajia kufanya kazi bega kwa bega na ninyi na wadau wengine katika mapambano dhidi ya UVIKO-19 na katika juhudi zetu thabiti za kuboresha usalama wa afya duniani,” alisema.


"Tunafurahi pia kusikia tangazo la Rais Samia Suluhu Hassan kwamba ana nia ya kuunda kikosi kazi cha kujifunza kuhusu UVIKO-19 na kutoa ushauri wa kisayansi wa namna ya kukabiliana nao kwa usahihi. Kwa kuongezea, Serikali ya Marekani inatumaini mrejeo wa ushahidi wa chanjo ni sehemu ya mchakato huo, na vile vile kujitolea kwa utoaji wa taarifa zilizoimarishwa pamoja na ushirikishwaji wa takwimu."

Kuomba taarifa zaidi, tafadhali piga simu Ubalozi wa Marekani Ofisi ya Habari Dar es Salaam Simu: +255 22 229-4000 au barua pepe: DPO@state.gov.

Image
Kwa mwaka jana, Marekani imetoa Dola milioni $ 16.4 kupunguza UVIKO-19 nchini Tanzania
Kwa mwaka jana, Marekani imetoa Dola milioni $ 16.4 kupunguza UVIKO-19 nchini Tanzania