Flag of Tanzania

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Language: English | Swahili

Speeches Shim

29-06-2021 11:30

DAR ES SALAAM-Leo, Serikali ya Marekani, kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), na Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija, Mkuu wa Wilaya ya Ilala wamekabidhi vifaa vya kuanzisha biashara vinavyoingiza kipato na samani za ofisini na vifaa vya kukusanya na kuhifadhi taarifa kwa wanufaika nchini.

Vifaa vya kuanzisha biashara vilitolewa kupitia mradi wa USAID wa Kizazi Kipya. Ufadhili wa vifaa hutoa njia kwa vijana kustawi katika fani walizosomea kama vile ushonaji, useremala, uashi, uokaji, ufundi bomba, urembo wa nywele, upishi, na uandaaji wa chakula. Kabla ya kupokea vifaa hivyo, Kizazi Kipya iliwasaidia vifaa vya kusomea na udhamini wa masomo kwa vijana kuhudhuria mafunzo ya ufundi katika vyuo vya mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), pamoja na vyuo vingine vilivyo na mamlaka ya kutoa mafunzo ya ustadi nchini Tanzania. Kwa jumla, Kizazi Kipya imesaidia vijana karibu 10,000 na udhamini wa ufundi na vifaa vya kuanzisha biashara kutoka halmashauri 81 katika mikoa 25 tangu mwaka 2018. Thamani ya jumla ya vifaa vya kuanzisha biashara vilivyokabidhiwa hadi sasa ni Shilingi za Kitanzania bilioni 15.2 (Dola za Marekani milioni 6.7).

Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dk. Donald Wright ametangaza msaada mpya kwa Wizara ya Afya ya Zanzibar kusaidia jitihada za kubaini na kushughulikia milipuko ya maradhi, hususan janga la COVID-19.
19-05-2021 12:15

Zanzibar – Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dk. Donald Wright leo ametangaza msaada mpya kwa Wizara ya Afya ya Zanzibar kusaidia jitihada za kubaini na kushughulikia milipuko ya maradhi, hususan janga la COVID-19.  Balozi Wright ametangaza msaada huo katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Uendeshaji Huduma za Dharura za Afya ya Jamii Zanzibar (Zanzibar Public Health Emergency Operations Center – ZPHEOC), kilichoanzishwa kwa msaada kutoka Kituo cha Udhibiti wa Maradhi cha Marekani (CDC), Shirika la Afya Duniani (WHO) na taasisi ya Global Fund.  Balozi Wright alifungua kituo hicho katika hafla iliyohudhuriwa pia na Waziri wa Afya wa Zanzibar Nassor Mazrui, Mwakilishi wa WHO, Dk. Ghirmay Andemichael na Mwakilishi wa Global Fund Nelson Msuya.

Kusherehekea Miaka Mitano ya ujifunzaji wa madarasa ya awali/chini, Hesabu na Elimu Jumuishi
21-04-2021 15:30

Dar es Salaam, Tanzania - Aprili 20, Serikali ya Marekani, kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), imeendesha kikao mubashara kwa njia ya mtandao kusherehekea mafanikio ya elimu ya msingi yaliyopatikana kwa miaka mitano ya mradi wa Tusome Pamoja na miaka miwili ya mradi wa Hesabu na Elimu Jumuishi.

Kama sehemu ya mkakati jumuishi wa udhibiti wa malaria, PMI inaendelea kuunga mkono utekelezaji wa Unyunyiziaji wa Dawa ya Ukoko Majumbani. Dawa ya ukoko majumbani huua mbu wanapofika maeneo yenye dawa, kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa malaria.
21-04-2021 10:15

Dar es Salaam, Tanzania - Mwaka jana, UVIKO-19 ilisababisha janga la kidunia ambalo halikutegemewa kutokea. Hata hivyo malaria imekuwa tatizo kwa muda mrefu nchini Tanzania. Marekani inajivunia kuisaidia Tanzania kuendelea na mapambano yake dhidi ya malaria. Jitihada ambazo Tanzania imechukua kuendeleza huduma muhimu za malaria zinaokoa maisha ya watu wengi.

Kwa mwaka jana, Marekani imetoa Dola milioni $ 16.4 kupunguza UVIKO-19 nchini Tanzania
20-04-2021 04:15

Mradi wa USAID wa Mnyororo wa Ugavi wa Afya Duniani hivi karibuni ulinunua vifaa vya upumuaji  na usafi wa mazingira vyenye thamani ya Dola za Marekani  $400,000. Vifaa viliwasilishwa mwezi uliopita Bandari ya Zanzibar na kusambazwa kwenye vituo vya umma vya kutolea huduma za afya kupitia bohari kuu ya madawa. Shehena hiyo inajumuisha vifaa vya kupumulia kama vile vipimo vya mwenendo wa damu, mirija ya kupimia puani kwa watoto na watu wazima, barakoa; na vifaa vya usafi wa mazingira kama vile dawa za mkoba za kunyunyizia, na mifuko ya kuwekea taka hatarishi.

 

USAID Kizazi Kipya itatumia mitandao yake iliyopo kutoa kadi za iCHF / iTIKA kwa kaya takriban 93,000 zilizo katika mazingira hatarishi na kwa jumla ya watu zaidi ya 360,000.
11-02-2021 04:15

Dodoma: Jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mheshimiwa Suleiman Jafo, alizindua mpango mpya wa kusambaza kadi za Mfuko wa Afya ya Jamii zilizoboreshwa (iCHF) / improved Tiba kwa Kadi (iTIKA) kwa kaya zilizo katika mazingira hatarishi. Kufikia kaya hizi, OR-TAMISEMI imeshirikiana na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) na Mpango wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI (PEPFAR), kupitia mradi wao wa Kizazi Kipya, ambao unasaidia yatima na watoto walio katika mazingira hatarishi.

Meneja wa Mazingira na Utafiti wa TMA Bi Sarah Osima akisaini hati rasmi ya makabidhiano ya vifaa vya hali ya hewa na Mratibu wa Mradi wa Kitaifa wa FAO Bwana Diomedes Kalisa (kulia) na Mratibu wa Nchini Bi. Rebecca Mwasyoke wa Ofisi ya Maendeleo ya Washington State University (kushoto). Tangu 2015, USAID imefadhili mradi wa “Building Capacity for Resilient Food Security," ambao hutoa msaada wa kitaalamu na ufadhili kwa TMA.
29-01-2021 00:45

Jumanne, Januari 19, Serikali ya Marekani, kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo ya Marekani, na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) walikabidhi zana za ufuatiliaji wa hali ya hewa kwa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA). Vifaa vyenyewe ni pamoja na vifaa vya kupima asidi na alkali, vifaa maalumu vya kupima mvua (vipima mvua), silinda za maabara za kupima ujazo wa vimiminika , kompyuta ya mezani, na uboreshaji wa seva mpya ya hifadhidata.

USAID PROTECT, mradi wa miaka mitano wa dola milioni 19.1, ulibuniwa katikati ya janga la ujangili lililoshuhudia Tanzania ikipoteza asilimia 60 ya idadi ya tembo nchini kati ya mwaka 2009 na 2014 pekee.
13-11-2020 01:15

Mradi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) wa Kuendeleza Mazingira, Uhifadhi, na Utalii wa Tanzania (PROTECT) ulifanya kikao mtandao kilichorushwa mubashara kusherehekea miaka mitano ya kulinda baioanuai na uchumi unaotokana na utalii.

Serikali ya Marekani yaimarisha mifumo ya afya inayolenga kumaliza janga la VVU nchini Tanzania
17-07-2020 04:30

Dar es salaam: Julai 16, wawakilishi kutoka Serikali ya Marekani na Serikali ya Tanzania walishiriki katika kikao-mtandao ambapo walijadili mafanikio na hatua za kuchukua siku zijazo ili kuimarisha  mifumo ya afya nchini Tanzania, kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) na mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Afya na Ustawi wa Jamii (CHSSP).

Fedha hizi ni nyongeza ya msaada wa Dola za Kimarekani milioni 1 unaolenga kusaidia mapambano dhidi ya janga la COVID-19 uliotolewa hivi karibuni na kufanya kiasi kipya cha fedha zilizotolewa kwa Tanzania ili kukabiliana na janga hili kufikia Dola za Kimarekani milioni 3.4.
22-05-2020 08:30

Dar es Salaam: Marekani imetangaza kuwa kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) itaongeza kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 2.4 (Takriban Shilingi za Kitanzania bilioni 5.6), ikiwa ni msaada kwa sekta ya afya nchini Tanzania.  Msaada huu unalenga kuimarisha uwezo wa maabara na upimaji wa kimaabara (laboratory capacity for optimal diagnostics), kusaidia jitihada za utoaji taarifa (risk communication) , miradi ya maji na usafi wa mazingira (water and sanitation), kuzuia na kudhibiti maambukizi,  kutoa elimu ya afya kwa umma (public health messaging) na miradi mingine. Fedha hizi ni nyongeza ya msaada wa Dola za Kimarekani milioni 1 unaolenga kusaidia mapambano dhidi ya janga la COVID-19 uliotolewa hivi karibuni na kufanya kiasi kipya cha fedha zilizotolewa kwa Tanzania ili kukabiliana na janga hili kufikia Dola za Kimarekani milioni 3.4. Isitoshe, kiasi kingine cha Dola za Kimarekani milioni 1.9 zimebadilishwa matumizi na kuelekezwa kwenye mapambano dhidi ya janga hili. Hii inafanya jumla ya fedha zote zilizotolewa na Marekani katika kukabiliana na COVID-19 nchini Tanzania hadi hivi sasa kufikia Dola za Kimarekani milioni 5.3 (Sawa na Shilingi za Kitanzania bilioni 12.2).

Last updated: August 16, 2021

Share This Page