Flag of Tanzania

Chumba cha Habari

Language: English | Swahili
22-08-2020

Tanzania imejaliwa kuwa na maliasili nyingi na imeweka kipaumbele katika kulinda usalama wa viumbe hai vyake kwa kuweka zaidi ya asilimia 32 ya eneo lake la ardhi kwenye uhifadhi. 

Serikali ya Marekani yaimarisha mifumo ya afya inayolenga kumaliza janga la VVU nchini Tanzania
17-07-2020

Dar es salaam: Julai 16, wawakilishi kutoka Serikali ya Marekani na Serikali ya Tanzania walishiriki katika kikao-mtandao ambapo walijadili mafanikio na hatua za kuchukua siku zijazo ili kuimarisha  mifumo ya afya nchini Tanzania, kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) na mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Afya na Ustawi wa Jamii (CHSSP).

Fedha hizi ni nyongeza ya msaada wa Dola za Kimarekani milioni 1 unaolenga kusaidia mapambano dhidi ya janga la COVID-19 uliotolewa hivi karibuni na kufanya kiasi kipya cha fedha zilizotolewa kwa Tanzania ili kukabiliana na janga hili kufikia Dola za Kimarekani milioni 3.4.
22-05-2020

Dar es Salaam: Marekani imetangaza kuwa kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) itaongeza kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 2.4 (Takriban Shilingi za Kitanzania bilioni 5.6), ikiwa ni msaada kwa sekta ya afya nchini Tanzania.  Msaada huu unalenga kuimarisha uwezo wa maabara na upimaji wa kimaabara (laboratory capacity for optimal diagnostics), kusaidia jitihada za utoaji taarifa (risk communication) , miradi ya maji na usafi wa mazingira (water and sanitation), kuzuia na kudhibiti maambukizi,  kutoa elimu ya afya kwa umma (public health messaging) na miradi mingine. Fedha hizi ni nyongeza ya msaada wa Dola za Kimarekani milioni 1 unaolenga kusaidia mapambano dhidi ya janga la COVID-19 uliotolewa hivi karibuni na kufanya kiasi kipya cha fedha zilizotolewa kwa Tanzania ili kukabiliana na janga hili kufikia Dola za Kimarekani milioni 3.4. Isitoshe, kiasi kingine cha Dola za Kimarekani milioni 1.9 zimebadilishwa matumizi na kuelekezwa kwenye mapambano dhidi ya janga hili. Hii inafanya jumla ya fedha zote zilizotolewa na Marekani katika kukabiliana na COVID-19 nchini Tanzania hadi hivi sasa kufikia Dola za Kimarekani milioni 5.3 (Sawa na Shilingi za Kitanzania bilioni 12.2).

20-09-2019

Mradi huu unakuza usawa wa kijinsia, ushiriki wa kisiasa, na uwezeshaji wa wanawake kuweza kupata nafasi muhimu za uongozi. USAID inakusudia kuhakikisha kuwa wanawake wanaongoza na kushiriki katika michakato ya kisiasa na uchaguzi-kama wapiga kura, wagombea, na wawakilishi waliochaguliwa. 

19-07-2018

On behalf of the United States Government, thank you all for joining us to launch these training efforts, which mark an important step forward in addressing gender-based violence and supporting safe learning environments. Gender-based violence remains a grave reality for countless women and youth in Tanzania and around the world, affecting victims regardless of socioeconomic status or background.

Last updated: October 26, 2020

Share This Page