Madhumuni ya mradi wa Feed the Future Tanzania Mboga na Matunda ni kufanya sehemu ndogo ya kilimo cha mazao ya bustani iwe na ushindani zaidi na jumuishi na kub        kuboresha hali ya lishe ya Watanzania kwa:

  • Kuongeza teknolojia zilizoboreshwa na mbinu za kuongeza tija kwa wakulima wadogo, kwa kuhusisha idadi kubwa ya wanawake na vijana katika bidhaa lengwa.
  • Kupanua mifumo ya soko inayoweza kufikia idadi kubwa ya walengwa wa moja kwa moja na wasio wa moja kwa moja, pamoja na watu walio katika mazingira magumu, na kuongeza biashara kwa bidhaa lengwa.
  • Kuimarisha uwezo wa jumla wa tasnia ya kilimo cha mazao ya bustani.